RAY C AMTEMBELEA RAIS KIKWETE
IKULU JIJINI DAR ES SALAAMAMSHUKURU
KWA MSAADA WA
MATIBABU
Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, alipofika Ikulu
ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada
mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini
ya uangalizi maalum.
Ray C alifika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth
Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa
ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na
hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya
uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili
aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea
katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu
anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake
rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake
za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.

No comments:
Post a Comment